Waefeso 5:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. Biblia Habari Njema - BHND maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. Neno: Bibilia Takatifu (kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), Neno: Maandiko Matakatifu (kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli), BIBLIA KISWAHILI kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; |
Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.
Ndugu zangu, mimi mwenyewe nina hakika juu yenu, kuwa ninyi mmejaa wema, na mmejazwa ujuzi wote, tena mnaweza kuonyana.
Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.
Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole.
Lakini kuhusu Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya haki.
ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,
Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.
Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.