Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Waefeso 5:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Biblia Habari Njema - BHND Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Neno: Bibilia Takatifu Ninyi wake, watiini waume zenu kama vile mnavyomtii Bwana Isa. Neno: Maandiko Matakatifu Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana Isa. BIBLIA KISWAHILI Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. |
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Basi mbiu ya mfalme atakayoipiga itakapotangazwa katika ufalme wake wote, nao ni mkubwa, wake wote watawaheshimu waume zao, wakubwa kwa wadogo.
Kwa maana alipeleka nyaraka katika majimbo yote ya mfalme, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake, ya kwamba kila mwanamume atawale nyumbani mwake, na kuitangaza habari hii kwa lugha ya watu wake.
Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba mnamtii Kristo;
Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu.
na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.