Waefeso 2:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu. Biblia Habari Njema - BHND Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu. Neno: Bibilia Takatifu si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu. Neno: Maandiko Matakatifu si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu. BIBLIA KISWAHILI wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. |
kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu.
(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),
Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.
ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu kabla ya wakati kuanza,