Waamuzi 9:48 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Abimeleki akakwea kwenda katika kilima cha Salmoni, yeye na wote waliokuwa pamoja naye; naye Abimeleki akashika shoka mkononi mwake, akakata tawi moja katika miti, akalishika na kujitwika begani mwake; akawaambia hao watu waliokuwa pamoja naye, “Haya, kile mlichoona nikifanya, nanyi fanyeni vivyo hivyo haraka”. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abimeleki na watu wake wakaenda mlimani Salmoni, akachukua shoka akakata tawi la mti na kuliweka begani mwake. Halafu akawaambia wale watu aliokuwa nao waharakishe kufanya kama alivyofanya. Biblia Habari Njema - BHND Abimeleki na watu wake wakaenda mlimani Salmoni, akachukua shoka akakata tawi la mti na kuliweka begani mwake. Halafu akawaambia wale watu aliokuwa nao waharakishe kufanya kama alivyofanya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abimeleki na watu wake wakaenda mlimani Salmoni, akachukua shoka akakata tawi la mti na kuliweka begani mwake. Halafu akawaambia wale watu aliokuwa nao waharakishe kufanya kama alivyofanya. Neno: Bibilia Takatifu yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Abimeleki akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua begani mwake. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Haraka! Fanyeni kile mmeona nikifanya!” Neno: Maandiko Matakatifu yeye na watu wake wote wakakwea kwenye Mlima Salmoni. Abimeleki akachukua shoka, akakata baadhi ya matawi, ambayo aliyachukua mabegani. Akawaagiza wale watu waliokuwa pamoja naye kuwa, “Fanyeni kile mlichoona mimi nikifanya!” BIBLIA KISWAHILI Basi Abimeleki akakwea kwenda katika kilima cha Salmoni, yeye na wote waliokuwa pamoja naye; naye Abimeleki akashika shoka mkononi mwake, akakata tawi moja katika miti, akalishika na kujitwika begani mwake; akawaambia hao watu waliokuwa pamoja naye, “Haya, kile mlichoona nikifanya, nanyi fanyeni vivyo hivyo haraka”. |
Basi watu hao wote wakakata kila mtu tawi lake, wakamfuata Abimeleki, wakayaweka hayo matawi pale ngomeni, na kuiteketeza moto hiyo ngome juu yao; ndipo watu wote wa huo mnara wa Shekemu wakafa, watu wapatao elfu moja, wanaume kwa wanawake.
Abimeleki akauendea huo mnara na kupigana nao; naye akaukaribia mlango wa mnara ili auteketeze.