Waamuzi 9:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi sasa, inuka wewe, usiku, wewe na watu walio pamoja nawe, mvizie mashambani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, rudi wewe na watu ulio nao, wakati wa usiku, uvizie mashambani karibu na mji. Biblia Habari Njema - BHND Basi, rudi wewe na watu ulio nao, wakati wa usiku, uvizie mashambani karibu na mji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, rudi wewe na watu ulio nao, wakati wa usiku, uvizie mashambani karibu na mji. Neno: Bibilia Takatifu Sasa basi, usiku huu wewe uondoke na watu wako ili mje kuwavizia mashambani. Neno: Maandiko Matakatifu Sasa, basi, usiku huu wewe uondoke na watu wako ili mje kuwavizia mashambani. BIBLIA KISWAHILI Basi sasa, inuka wewe, usiku, wewe na watu walio pamoja nawe, mvizie mashambani; |
Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
Basi Yoshua akainuka, na watu wote wa vita pamoja naye, ili waende Ai; Yoshua akachagua watu elfu thelathini, watu mashujaa wenye uwezo, akawatuma wakati wa usiku.
Akawaagiza, akasema, Angalieni, mtaotea kuuvizia ule mji, upande wa nyuma wa mji; msiende mbali sana na mji, lakini kaeni tayari nyote;
Naye akatuma wajumbe waende kwa Abimeleki kwa siri, akasema, Tazama, Gaali, mwana wa Ebedi, na ndugu zake wamekuja Shekemu; na wanaufitinisha mji huu kinyume chako.
kisha asubuhi na mapema, mara tu baada ya jua kuchomoza, inuka na uushambulie mji huo; na Gaali na wale watu walio pamoja naye watakapotokeza nje kupigana nawe, ndipo utakapowatenda kama utakavyoweza.