Waamuzi 9:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC lakini ikiwa basi moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini, kama sivyo, moto na utoke kwa Abimeleki na kuwateketeza wananchi wa Shekemu na Beth-milo, tena moto utoke kwa wananchi wa Shekemu na Beth-milo na kumteketeza Abimeleki.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini, kama sivyo, moto na utoke kwa Abimeleki na kuwateketeza wananchi wa Shekemu na Beth-milo, tena moto utoke kwa wananchi wa Shekemu na Beth-milo na kumteketeza Abimeleki.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini, kama sivyo, moto na utoke kwa Abimeleki na kuwateketeza wananchi wa Shekemu na Beth-milo, tena moto utoke kwa wananchi wa Shekemu na Beth-milo na kumteketeza Abimeleki.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini kama sivyo, moto na utoke kwa Abimeleki na uwateketeze, ninyi wenyeji wa Shekemu na Beth-Milo; nao moto utoke kwenu, wenyeji wa Shekemu na Beth-Milo, na umteketeze Abimeleki!” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kama sivyo, moto na utoke kwa Abimeleki na uwateketeze, ninyi watu wa Shekemu na Beth-Milo, nao moto utoke kwenu, watu wa Shekemu na Beth-Milo umteketeze Abimeleki!” BIBLIA KISWAHILI lakini ikiwa sivyo, moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki. |
Uwape sawasawa na vitendo vyao, Na kwa kadiri ya uovu wa matendo yao, Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao, Uwalipe kile wanachostahili.
Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuelekea Serera, hadi mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.
Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Ikiwa kwa kweli mnanitia mafuta niwe mfalme juu yenu, basi njoni mkakae chini ya kivuli changu; la sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.
basi ikiwa mmemtendea kwa nia njema na uzingativu Yerubaali na nyumba yake hivi leo, basi mfurahieni huyo huyo Abimeleki, yeye naye na awafurahie ninyi;
Kisha Yothamu akaenda zake na kukimbia, akaenda Beeri, na kukaa kuko, kwa kumwogopa Abimeleki nduguye.
Kisha Mungu akatuma roho mbaya kati ya Abimeleki na watu wa Shekemu; nao watu wa Shekemu wakamtendea Abimeleki kwa udanganyifu;
Abimeleki, na vile vikosi vilivyokuwa pamoja naye, wakafululiza, wakasimama penye maingilio ya lango la mji, na vile vikosi viwili vikawarukia hao wote waliokuwa mashambani, na kuwaua.
Kisha hao watu wote wa Shekemu wakakusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na kumtawaza Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo katika Shekemu.