Waamuzi 9:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC nanyi mmeinuka juu ya nyumba ya baba yangu hivi leo nanyi mmewaua wanawe, watu sabini, juu ya jiwe moja, nanyi mmemtawaza Abimeleki, mwana wa kijakazi chake, awe mfalme juu ya watu wa Shekemu kwa sababu yeye ni ndugu yenu;) Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini leo mmeishambulia jamaa ya baba yangu na kuwaua wana sabini juu ya jiwe moja, halafu mmemfanya Abimeleki mtoto wa mjakazi wa baba, awe mfalme wa wakazi wa Shekemu kwa sababu tu ni mtu wa ukoo wenu. Biblia Habari Njema - BHND Lakini leo mmeishambulia jamaa ya baba yangu na kuwaua wana sabini juu ya jiwe moja, halafu mmemfanya Abimeleki mtoto wa mjakazi wa baba, awe mfalme wa wakazi wa Shekemu kwa sababu tu ni mtu wa ukoo wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini leo mmeishambulia jamaa ya baba yangu na kuwaua wana sabini juu ya jiwe moja, halafu mmemfanya Abimeleki mtoto wa mjakazi wa baba, awe mfalme wa wakazi wa Shekemu kwa sababu tu ni mtu wa ukoo wenu. Neno: Bibilia Takatifu lakini leo mmeasi dhidi ya jamaa ya baba yangu, na kuwaua wanawe sabini juu ya jiwe moja. Nanyi mmemtawaza Abimeleki mwana wa mjakazi wake kuwa mfalme juu ya wenyeji wa Shekemu, kwa kuwa yeye ni ndugu yenu. Neno: Maandiko Matakatifu (lakini leo mmeasi dhidi ya jamaa ya baba yangu, na kuwaua wanawe sabini juu ya jiwe moja, nanyi mkamfanya Abimeleki mwana wa mwanamke mtumwa kuwa mfalme juu ya Shekemu, kwa kuwa yeye ni ndugu yenu), BIBLIA KISWAHILI nanyi mmeinuka juu ya nyumba ya baba yangu hivi leo nanyi mmewaua wanawe, watu sabini, juu ya jiwe moja, nanyi mmemtawaza Abimeleki, mwana wa kijakazi chake, awe mfalme juu ya watu wa Shekemu kwa sababu yeye ni ndugu yenu;) |
wala hawakuifanyia mema nyumba ya Yerubaali, yaani Gideoni, licha ya hayo mema yote aliyowafanyia Waisraeli.
(kwa maana baba yangu aliwatetea ninyi, na kuhatarisha uhai wake, na kuwaokoa na mikono ya Midiani;
basi ikiwa mmemtendea kwa nia njema na uzingativu Yerubaali na nyumba yake hivi leo, basi mfurahieni huyo huyo Abimeleki, yeye naye na awafurahie ninyi;
Haya, neneni tafadhali masikioni mwa wanaume wote wa Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo bora kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali wote, ambao ni watu sabini, wawatawale, au kwamba mtu mmoja awatawale? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.