Naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ulituma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni, kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.
Waamuzi 9:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwishowe miti yote ikauendea mti wa miiba na kuuambia, ‘Njoo wewe utawale juu yetu.’ Biblia Habari Njema - BHND Mwishowe miti yote ikauendea mti wa miiba na kuuambia, ‘Njoo wewe utawale juu yetu.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwishowe miti yote ikauendea mti wa miiba na kuuambia, ‘Njoo wewe utawale juu yetu.’ Neno: Bibilia Takatifu “Mwishoni miti yote ikauambia mchongoma, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’ Neno: Maandiko Matakatifu “Mwishoni miti yote ikauambia mti wa miiba, ‘Njoo na uwe mfalme wetu.’ BIBLIA KISWAHILI Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu. |
Naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ulituma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni, kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.
Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayumbayumbe juu ya miti?
Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Ikiwa kwa kweli mnanitia mafuta niwe mfalme juu yenu, basi njoni mkakae chini ya kivuli changu; la sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.