Naye mfalme akaapa, akasema, BWANA aishivyo, aliyenikomboa roho yangu katika shida zote,
Waamuzi 8:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye akasema, Watu hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu; kama yeye BWANA aishivyo, kama mngaliwaokoa hai watu hao, nami nisingewaua ninyi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye akawaambia, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu mzazi. Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, kama msingewaua, hata mimi nisingewaua.” Biblia Habari Njema - BHND Naye akawaambia, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu mzazi. Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, kama msingewaua, hata mimi nisingewaua.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye akawaambia, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu mzazi. Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, kama msingewaua, hata mimi nisingewaua.” Neno: Bibilia Takatifu Gideoni akajibu, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu hasa. Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, kama mngekuwa mmewaacha hai, mimi nisingewaua ninyi.” Neno: Maandiko Matakatifu Gideoni akajibu, “Hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu hasa. Hakika kama aishivyo bwana, kama mngekuwa mmewaacha hai, mimi nisingewaua ninyi.” BIBLIA KISWAHILI Naye akasema, Watu hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu; kama yeye BWANA aishivyo, kama mngaliwaokoa hai watu hao, nami nisingewaua ninyi. |
Naye mfalme akaapa, akasema, BWANA aishivyo, aliyenikomboa roho yangu katika shida zote,
Mwenye kutwaa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji; hapo atakapokutana naye, atamwua.
Ndipo akawaambia hao Zeba na Salmuna, Hao watu mliowaua huko Tabori walikuwa watu wa namna gani? Wakamjibu, Walikuwa kama wewe ulivyo; kila mmoja alikuwa anafanana na wana wa mfalme.
Kisha akamwambia Yetheri mwanawe mzaliwa wa kwanza, Haya, simama, uwaue hawa. Lakini huyo kijana hakutoa upanga wake; maana, akaogopa, kwa sababu alikuwa ni kijana tu.
Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; BWANA aishivyo. Ulale wewe hadi asubuhi.