Waamuzi 6:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli walidhoofishwa sana na Wamidiani hata wakamlilia Mwenyezi-Mungu awasaidie. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli walidhoofishwa sana na Wamidiani hata wakamlilia Mwenyezi-Mungu awasaidie. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli walidhoofishwa sana na Wamidiani hata wakamlilia Mwenyezi-Mungu awasaidie. Neno: Bibilia Takatifu Wamidiani wakaifanya Israeli kuwa maskini sana, hata Waisraeli wakamlilia Mwenyezi Mungu kumwomba msaada. Neno: Maandiko Matakatifu Waisraeli wakafanywa kuwa maskini sana na Wamidiani, hata Israeli wakamlilia bwana kuomba msaada. BIBLIA KISWAHILI Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia BWANA. |
BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.
Nao watakula mavuno yako, na mkate wako, ambao iliwapasa wana wako na binti zako kuula; watakula makundi yako ya kondoo na ya ng'ombe; watakula mizabibu yako na mitini yako; wataiharibu miji yako yenye boma, uliyokuwa ukiitumainia, naam, wataiharibu kwa upanga.
Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwapondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; BWANA wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao BWANA anawaghadhabikia milele.
Ndipo wana wa Israeli wakamlilia BWANA, wakisema, Sisi tumekufanyia dhambi, kwa sababu tumemuacha Mungu wetu, na kuyatumikia Mabaali.
Lakini wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi.
Kisha wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa ya vita; naye akawakandamiza sana wana wa Israeli muda wa miaka ishirini.