Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa moyo wao wote, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea BWANA; mfalme Daudi naye akafurahi sana.
Waamuzi 5:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wangu unawaelekea makamanda wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nawapa heshima makamanda wa Israeli waliojitoa kwa hiari yao kati ya watu. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu! Biblia Habari Njema - BHND Nawapa heshima makamanda wa Israeli waliojitoa kwa hiari yao kati ya watu. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nawapa heshima makamanda wa Israeli waliojitoa kwa hiari yao kati ya watu. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu! Neno: Bibilia Takatifu Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, u pamoja na wale wanaojitoa kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini Mwenyezi Mungu! Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, pamoja na wale wanaojitoa wenyewe kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini bwana! BIBLIA KISWAHILI Moyo wangu unawaelekea makamanda wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini BWANA. |
Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa moyo wao wote, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea BWANA; mfalme Daudi naye akafurahi sana.
na baada yake Amasia mwana wa Zikri, aliyejitoa kwa BWANA kwa moyo, na pamoja naye elfu mia mbili, watu mashujaa;
Hata walipokuja Hezekia na wakuu, na kuyaona yale mafungu, wakamhimidi BWANA, na watu wake Israeli.
Watu wako watajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.
Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.
Maana aliyapokea kweli yale maonyo; tena, huku akizidi kuwa na bidii, alisafiri kwenda kwenu kwa hiari yake mwenyewe.
Basi niliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa nguvu.
Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli, Kwa sababu watu walijitoa nafsi zao kwa hiari yao, Mhimidini BWANA.