Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Waamuzi 5:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Watawala walikoma katika Israeli, walikoma, Hadi mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wakulima walikoma kuwako, walikoma kuwako katika Israeli, mpaka nilipotokea mimi Debora, mimi niliye kama mama wa Israeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wakulima walikoma kuwako, walikoma kuwako katika Israeli, mpaka nilipotokea mimi Debora, mimi niliye kama mama wa Israeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wakulima walikoma kuwako, walikoma kuwako katika Israeli, mpaka nilipotokea mimi Debora, mimi niliye kama mama wa Israeli.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma hadi mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Watawala walikoma katika Israeli, walikoma, Hadi mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Waamuzi 5:7
7 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi ni mmoja wa hao wenye amani, walio waaminifu katika Israeli; wewe unataka kuuharibu mji ulio kama mama wa Israeli; mbona unataka kuumeza urithi wa BWANA?

Kwa sababu hii Wayahudi wa vijijini, wakaao katika miji isiyo na ngome, huishika siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, kuwa siku ya furaha na karamu, sikukuu ya kupelekeana zawadi.

Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.

Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia.

Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi, Siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina watu; Nayo misafara ilipita kwa njia za kando.

Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arubaini wa Israeli?