Waamuzi 5:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Milima ikayeyuka mbele za uso wa BWANA, Naam hata Sinai ule mbele za uso wa BWANA, Mungu wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Milima ilitikisika mbele yako Mwenyezi-Mungu, naam, mlima Sinai mbele yako Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Milima ilitikisika mbele yako Mwenyezi-Mungu, naam, mlima Sinai mbele yako Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Milima ilitikisika mbele yako Mwenyezi-Mungu, naam, mlima Sinai mbele yako Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Milima ilitetemeka mbele za Mwenyezi Mungu, Yule wa Sinai, mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Milima ilitetemeka mbele za bwana, hata ule wa Sinai, mbele za bwana, Mungu wa Israeli. BIBLIA KISWAHILI Milima ikayeyuka mbele za uso wa BWANA, Naam hata Sinai ule mbele za uso wa BWANA, Mungu wa Israeli. |
Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.
Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuri, mlima wote ukatetemeka sana.
Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali.
Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.
Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.
Maana hamkufikia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,