Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandalia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
Waamuzi 5:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aliomba maji, naye akampa maziwa. Akamletea siagi katika sahani ya heshima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa; alimletea siagi katika bakuli ya heshima. Biblia Habari Njema - BHND Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa; alimletea siagi katika bakuli ya heshima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa; alimletea siagi katika bakuli ya heshima. Neno: Bibilia Takatifu Sisera alimwomba maji, naye akampa maziwa; kwenye bakuli la heshima akamletea maziwa mgando. Neno: Maandiko Matakatifu Aliomba maji, naye akampa maziwa; kwenye bakuli la heshima akamletea maziwa mgando. BIBLIA KISWAHILI Aliomba maji, naye akampa maziwa. Akamletea siagi katika sahani ya heshima. |
Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandalia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote; Mkewe Heberi, Mkeni, Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani.
Akanyosha mkono wake akashika kigingi, Nao mkono wake wa kulia ukashika nyundo ya fundi; Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake. Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake.