Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
Waamuzi 5:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote; Mkewe Heberi, Mkeni, Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Abarikiwe kuliko wanawake wote Yaeli, mke wa Heberi, Mkeni. Naam, amebarikiwa kuliko wanawake wote wanaokaa mahemani. Biblia Habari Njema - BHND “Abarikiwe kuliko wanawake wote Yaeli, mke wa Heberi, Mkeni. Naam, amebarikiwa kuliko wanawake wote wanaokaa mahemani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Abarikiwe kuliko wanawake wote Yaeli, mke wa Heberi, Mkeni. Naam, amebarikiwa kuliko wanawake wote wanaokaa mahemani. Neno: Bibilia Takatifu “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, mkewe Heberi, Mkeni, abarikiwe kuliko wanawake wote wanaoishi kwenye mahema. Neno: Maandiko Matakatifu “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, mkewe Heberi, Mkeni, abarikiwe kuliko wanawake wote waishio kwenye mahema. BIBLIA KISWAHILI Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote; Mkewe Heberi, Mkeni, Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani. |
Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.
Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika.