Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawajaribu huko;
Waamuzi 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za BWANA, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu alikusudia kuwatumia hao ili awajaribu Waisraeli, aone kama watatii amri zake alizowaamuru wazee wao kwa njia ya Mose. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu alikusudia kuwatumia hao ili awajaribu Waisraeli, aone kama watatii amri zake alizowaamuru wazee wao kwa njia ya Mose. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu alikusudia kuwatumia hao ili awajaribu Waisraeli, aone kama watatii amri zake alizowaamuru wazee wao kwa njia ya Mose. Neno: Bibilia Takatifu Waliachwa ili kuwajaribu Waisraeli, kuona kama wangetii amri za Mwenyezi Mungu, alizokuwa amewapa baba zao kwa mkono wa Musa. Neno: Maandiko Matakatifu Waliachwa ili kuwajaribu Waisraeli kuona kama wangetii amri za bwana, alizokuwa amewapa baba zao kwa mkono wa Musa. BIBLIA KISWAHILI Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua kwamba watasikiliza amri za BWANA, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa. |
Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawajaribu huko;
Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.
Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu Israeli, kama wataifuata njia ya BWANA kwenda katika njia hiyo, au sivyo.
Basi haya ndiyo mataifa ambao BWANA aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani, awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani;