Kisha akamsogezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyenenepa sana.
Waamuzi 3:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye hapo alipomaliza kuitoa hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua tunu, wakaenda zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ehudi alipomaliza kutoa zawadi, akawaambia watu waliobeba zawadi, waondoke. Biblia Habari Njema - BHND Ehudi alipomaliza kutoa zawadi, akawaambia watu waliobeba zawadi, waondoke. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ehudi alipomaliza kutoa zawadi, akawaambia watu waliobeba zawadi, waondoke. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Ehudi kumkabidhi ule ushuru, akawatuma wale watu waliokuwa wameubeba huo ushuru waende zao. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Ehudi kumkabidhi ule ushuru, wale watu waliokuwa wameubeba huo ushuru aliwaruhusu waende zao. BIBLIA KISWAHILI Naye hapo alipomaliza kuitoa hiyo tunu, akawapa ruhusa watu hao walioichukua tunu, wakaenda zao. |
Kisha akamsogezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyenenepa sana.
Lakini yeye mwenyewe akageuka kutoka huko kwenye sanamu zilizokuwa karibu na Gilgali, akasema, Mimi nina ujumbe wa siri kwako wewe, Ee mfalme. Naye akasema, Nyamazeni kimya. Watu wote waliokuwa wanasimama karibu naye wakatoka na kumwacha.