Ikapigwa mbiu jeshini, jua likichwa, kusema, Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake.
Waamuzi 21:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wana wa Israeli wakati huo wakaenda zao, kila mtu akaenda kwa kabila yake na kwa jamaa yake; nao wakatoka huko, waende kila mtu kuuendea urithi wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huohuo Waisraeli wakaondoka, kila mtu akarudi katika eneo la kabila lake na jamaa yake. Kila mtu alirudi katika sehemu aliyogawiwa. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huohuo Waisraeli wakaondoka, kila mtu akarudi katika eneo la kabila lake na jamaa yake. Kila mtu alirudi katika sehemu aliyogawiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huohuo Waisraeli wakaondoka, kila mtu akarudi katika eneo la kabila lake na jamaa yake. Kila mtu alirudi katika sehemu aliyogawiwa. Neno: Bibilia Takatifu Wakati huo Waisraeli wakaondoka sehemu ile na kwenda nyumbani kwao, kwa makabila yao na kwa jamaa zao, kila mmoja kwenye urithi wake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huo Waisraeli wakaondoka sehemu ile na kwenda nyumbani kwao, kwenye makabila yao na kwa jamaa zao, kila mmoja kwenye urithi wake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Nao wana wa Israeli wakati huo wakaenda zao, kila mtu akaenda kwa kabila lake na kwa jamaa yake; nao wakatoka huko, waende kila mtu kuuendea urithi wake. |
Ikapigwa mbiu jeshini, jua likichwa, kusema, Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake.
Wana wa Benyamini wakafanya hivyo, wakajitwalia wake, kulingana na hesabu yao, katika hao waliocheza, wakawachukua wakaenda nao; kisha wakaenda kuurudia urithi wao, na kuijenga miji na kuishi humo.
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya yaliyokuwa ni mema machoni pake mwenyewe.