Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Waamuzi 21:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kisha baba zao au ndugu zao watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa hisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; na kwa kuwa hamkuwapa wao, la sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Baba zao au kaka zao wakija kutulalamikia tutawaambia, “Sisi tunawaombeni mwahurumie watu wa Benyamini na kuwaachia wawachukue hao wanawake; maana hatukuwapata katika vita vya Yabesh-gileadi. Na kwa vile nyinyi wenyewe hamkutupatia hao binti zenu, hamtahukumiwa.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Baba zao au kaka zao wakija kutulalamikia tutawaambia, “Sisi tunawaombeni mwahurumie watu wa Benyamini na kuwaachia wawachukue hao wanawake; maana hatukuwapata katika vita vya Yabesh-gileadi. Na kwa vile nyinyi wenyewe hamkutupatia hao binti zenu, hamtahukumiwa.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Baba zao au ndugu zao watakapotulalamikia, tutawaambia, ‘Kuweni wakarimu kwetu, nanyi mturuhusu tuwe nao kwa kuwa hatukuweza kumpa kila mtu mke tulipopigana. Lakini ninyi pia hamna hatia, kwa kuwa hamkuwapa wao binti zenu kuwa wake.’ ”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Baba zao au ndugu zao waume watakapotulalamikia, tutawaambia, ‘Kuweni wakarimu kwetu, nanyi mturuhusu tuwe nao kwa kuwa hatukuweza kumpa kila mtu mke tulipopigana. Lakini ninyi pia hamna hatia kwa kuwa hamkuwapa wao binti zenu kuwa wake.’ ”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kisha baba zao au ndugu zao watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa hisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; na kwa kuwa hamkuwapa wao, la sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Waamuzi 21:22
10 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye;

Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu; Na baada ya kuweka nadhiri kuulizauliza habari.

Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

Basi watu wa Israeli walikuwa wameapa huko katika Mispa, wakisema, Hapana mtu yeyote kwetu sisi atakayemwoza binti yake kumpa Benyamini.

Basi Benyamini wakarudi wakati huo; kisha wakawapa wale wanawake waliowasalimisha katika hao wanawake wa Yabesh-gileadi; lakini wanawake hao hawakuwatosha.

Lakini sisi hatuwezi kuwaoza binti zetu kwa maana wana wa Israeli walikuwa wameapa, wakisema, Na alaaniwe huyo atakayempa Benyamini mke.

Tufanyeje sisi ili tuwapatie wake hao waliosalia, kwa kuwa tumeapa kwa BWANA ya kwamba hatutawapa binti zetu ili wawaoe?