Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
Waamuzi 21:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Benyamini wakarudi wakati huo; kisha wakawapa wale wanawake waliowasalimisha katika hao wanawake wa Yabesh-gileadi; lakini wanawake hao hawakuwatosha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanaume hao wa kabila la Benyamini wakawarudia hao wenzao wakati huohuo. Basi wakapewa wale wanawake ambao walikuwa wamesalimishwa huko Yabesh-gileadi. Lakini wanawake hao hawakuwatosha. Biblia Habari Njema - BHND Wanaume hao wa kabila la Benyamini wakawarudia hao wenzao wakati huohuo. Basi wakapewa wale wanawake ambao walikuwa wamesalimishwa huko Yabesh-gileadi. Lakini wanawake hao hawakuwatosha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanaume hao wa kabila la Benyamini wakawarudia hao wenzao wakati huohuo. Basi wakapewa wale wanawake ambao walikuwa wamesalimishwa huko Yabesh-gileadi. Lakini wanawake hao hawakuwatosha. Neno: Bibilia Takatifu Basi Wabenyamini wakarudi wakati ule, nao wakapewa wale wanawali wa Yabesh-Gileadi waliohifadhiwa. Lakini hawakuwatosha wanaume wote. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Wabenyamini wakarudi nyumbani mwao, wakapewa wale wanawali wa Yabeshi-Gileadi waliowaponya. Lakini hawakuwatosha wanaume wote. BIBLIA KISWAHILI Basi Benyamini wakarudi wakati huo; kisha wakawapa wale wanawake waliowasalimisha katika hao wanawake wa Yabesh-gileadi; lakini wanawake hao hawakuwatosha. |
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
Lakini wanaume mia sita wakageuka, wakakimbilia upande wa nyikani hadi katika jabali la Rimoni, wakakaa kwenye hilo jabali la Rimoni muda wa miezi minne.
Nao wakapata katika wenyeji wa Yabesh-gileadi wanawali mia nne, ambao hawajamjua mwanamume kwa kulala naye; basi wakawaleta kambini huko Shilo, ulioko katika nchi ya Kanaani.
Basi mkutano ukatuma watu na kunena na wana wa Benyamini waliokuwako huko katika jabali la Rimoni, wakawatangazia amani.
Nao watu wakawahurumia Wabenyamini, kwa sababu BWANA alikuwa amefanya pengo katika hayo makabila ya Israeli.
Kisha baba zao au ndugu zao watakapokuja kushitaki, sisi tutawaambia, Kwa hisani yenu tupeni sisi; kwa kuwa hatukumtwalia kila mtu mkewe katika vita; na kwa kuwa hamkuwapa wao, la sivyo ninyi sasa mngekuwa na hatia.
Basi wakasema, Ni ipi katika makabila ya Israeli ambayo haikufika mbele ya Bwana huko Mispa.