Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Waamuzi 20:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nao wanaume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walitaka kuniua, na suria wangu wakambaka nguvu, hata amekufa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini watu wa mji wa Gibea wakaja usiku wakaizingira nyumba nilimokuwa nimelala. Walitaka kuniua, wakambaka suria wangu mpaka akafa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini watu wa mji wa Gibea wakaja usiku wakaizingira nyumba nilimokuwa nimelala. Walitaka kuniua, wakambaka suria wangu mpaka akafa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini watu wa mji wa Gibea wakaja usiku wakaizingira nyumba nilimokuwa nimelala. Walitaka kuniua, wakambaka suria wangu mpaka akafa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wakati wa usiku wanaume wa Gibea wakanijia na kuizingira nyumba, wakitaka kuniua. Wakambaka suria wangu hata akafa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakati wa usiku watu wa Gibea wakanijia na kuizingira nyumba, wakitaka kuniua. Wakambaka suria wangu mpaka akafa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nao wanaume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walitaka kuniua, na suria wangu wakambaka nguvu, hata akafa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Waamuzi 20:5
10 Marejeleo ya Msalaba  

Msijitie unajisi katika hata mojawapo ya mambo hayo; kwa maana hayo mataifa nitakayoyatoa mbele zenu yamekuwa najisi kwa mambo hayo yote;


na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na wanaume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.


watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga ukelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.


Tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la BWANA, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli.


Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu mabaradhuli wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua.


Akamwambia, Haya inuka, twende zetu; lakini hakumjibu; ndipo akamwinua akamweka juu ya punda; mtu huyo akaondoka, akaenda kwake nyumbani.


Huyo Mlawi, huyo mume wa mwanamke aliyeuawa, akajibu na kusema, Mimi nilifika Gibea ulio wa Benyamini mimi na suria yangu, ili tulale.