Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya mataifa, Haoni raha yoyote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake.
Waamuzi 20:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa hiyo wakageuza maungo yao mbele ya wana wa Israeli kuelekea njia ya kwenda nyikani; lakini ile vita ikawaandamia kwa kasi; na hao waliotoka katika ile miji wakawaangamiza katikati yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo wakageuka, wakawakimbia Waisraeli kuelekea jangwani, lakini vita vikawakumba; wakajikuta wako katikati ya majeshi mawili ya Israeli, na askari waliotoka wakawaangamiza. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo wakageuka, wakawakimbia Waisraeli kuelekea jangwani, lakini vita vikawakumba; wakajikuta wako katikati ya majeshi mawili ya Israeli, na askari waliotoka wakawaangamiza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo wakageuka, wakawakimbia Waisraeli kuelekea jangwani, lakini vita vikawakumba; wakajikuta wako katikati ya majeshi mawili ya Israeli, na askari waliotoka wakawaangamiza. Neno: Bibilia Takatifu Basi wakakimbia mbele ya Waisraeli kuelekea nyikani, lakini hawakuweza kukwepa vile vita. Nao Waisraeli waliotoka katika ile miji wakawaua huko. Neno: Maandiko Matakatifu Basi wakakimbia mbele ya Waisraeli kuelekea nyikani, lakini hawakuweza kukwepa vile vita. Nao watu wa Israeli waliotoka katika ile miji wakawaua huko. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo wakageuza maungo yao mbele ya wana wa Israeli kuelekea njia ya kwenda nyikani; lakini ile vita ikawaandamia kwa kasi; na hao waliotoka katika ile miji wakawaangamiza katikati yake. |
Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya mataifa, Haoni raha yoyote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake.
Ee Israeli, umefanya dhambi tangu siku za Gibea; huko ndiko walikosimama; Je, vita juu ya wana wa uovu hakitawapata katika Gibea?
Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.
Kisha Yoshua na watu wa Israeli wote walifanya kana kwamba wameshindwa mbele yao, wakakimbia kwa njia ya nyika.
Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamekwisha kuwaua wenyeji wote wa Ai katika bara, hapo katika nyika walipokuwamo wakiwafuatia, nao walikuwa wamekwisha anguka wote kwa makali ya upanga, hadi walipokuwa wameangamizwa wote, ndipo Israeli wakarejea Ai, na kuupiga huo mji kwa makali ya upanga.