Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Waamuzi 20:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anasimama mbele ya hilo sanduku siku hizo), wakasema, Je! Nitoke tena niende kupigana na wana wa Benyamini ndugu yangu, au niache? BWANA akawaambia, Haya, kweeni; kwa kuwa kesho nitamtoa na kumtia mkononi mwako.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Aroni alikuwa na wajibu wa kuhudumu mbele yake. Waisraeli wakamwuliza Mwenyezi-Mungu, “Je, twende tena kupigana na ndugu zetu, watu wa kabila la Benyamini?” Mwenyezi-Mungu akawaambia, “Nendeni. Kesho nitawatia mikononi mwenu.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Aroni alikuwa na wajibu wa kuhudumu mbele yake. Waisraeli wakamwuliza Mwenyezi-Mungu, “Je, twende tena kupigana na ndugu zetu, watu wa kabila la Benyamini?” Mwenyezi-Mungu akawaambia, “Nendeni. Kesho nitawatia mikononi mwenu.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

na Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anahudumu mbele za hilo Sanduku.) Wakauliza, “Je, tupande tena kwenda vitani kupigana na Wabenyamini, ndugu zetu, au la?” Mwenyezi Mungu akajibu, “Nendeni, kwa kuwa kesho nitawatia mikononi mwenu.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

na Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anahudumu mbele za hilo Sanduku.) Wakauliza, “Je, tupande kwenda vitani kupigana tena na Wabenyamini ndugu zetu, au la?” bwana akajibu, “Nendeni, kwa kuwa kesho nitawatia mikononi mwenu.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anasimama mbele ya hilo sanduku siku hizo), wakasema, Je! Nitoke tena niende kupigana na wana wa Benyamini ndugu yangu, au niache? BWANA akawaambia, Haya, kweeni; kwa kuwa kesho nitamtoa na kumtia mkononi mwako.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Waamuzi 20:28
21 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya.

Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa BWANA yuko pamoja nanyi.

mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, kuhani mkuu;

Na Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja miongoni mwa binti za Putieli; naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba wa Walawi kulingana na jamaa zao.

Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu.

Na wakati huo BWANA alilitenga kabila la Lawi ili walichukue lile sanduku la Agano la BWANA, wasimame mbele ya BWANA kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.

Kwani BWANA, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la BWANA, yeye na wanawe milele.

Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, hadi nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani;

Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika Gibea, mji wa Finehasi mwanawe, ambao alipewa katika nchi ya vilima ya Efraimu.

Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tu, tungaliridhika kukaa ng'ambo ya Yordani

BWANA akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake.

Kisha, tazama, akatokea mwanamume mzee, akitoka kazini kwake shambani, wakati wa jioni; mtu huyo alikuwa ni wa ile nchi ya vilima vilima ya Efraimu, naye alikuwa anakaa katika Gibea kama mgeni lakini wenyeji wa mahali hapo walikuwa Wabenyamini.

Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako.

Basi Sauli akataka shauri kwa Mungu, Je! Nishuke ili kuwafuatia Wafilisti? Je! Utawatia mikononi mwa Israeli? Lakini hakumjibu neno lolote siku ile.

Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.