Lakini Yeroboamu aliwazungushia waviziao kwa nyuma; basi wao wakawa mbele ya Yuda, na wale waviziao nyuma yao.
Waamuzi 20:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini wana wa Benyamini wakakutanika huko Gibea kutoka katika miji yao, ili watoke kwenda kupigana na wana wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi walikusanyika huko Gibea kutoka katika kila mji wao, ili kupigana na Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Basi walikusanyika huko Gibea kutoka katika kila mji wao, ili kupigana na Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi walikusanyika huko Gibea kutoka katika kila mji wao, ili kupigana na Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu Wakatoka katika miji yao, wakakutanika Gibea ili kupigana na Waisraeli. Neno: Maandiko Matakatifu Wakatoka katika miji yao, wakakutanika Gibea ili kupigana na Waisraeli. BIBLIA KISWAHILI Lakini wana wa Benyamini wakakutanika huko Gibea kutoka katika miji yao, ili watoke kwenda kupigana na wana wa Israeli. |
Lakini Yeroboamu aliwazungushia waviziao kwa nyuma; basi wao wakawa mbele ya Yuda, na wale waviziao nyuma yao.
Akamwambia, Hutapita katika nchi yangu. Kisha Edomu akamtokea ili kupigana naye, na watu wengi, na kwa mkono wa nguvu.
Lakini Sihoni hakukubali kumwacha Israeli kupita katika mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, akatoka aende kupigana na Israeli jangwani, akafika mpaka Yahasa; akapigana na Israeli.
Basi sasa watoeni watu hao, hao mabaradhuli walio katika Gibea, ili tuwaue, na kuuondoa uovu katika Israeli. Lakini Benyamini hawakukubali kuisikia sauti ya ndugu zao wana wa Israeli.
Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, wanaume elfu ishirini na sita waliokuwa na silaha, mbali na hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.