Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Waamuzi 2:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kisha BWANA akawainua waamuzi, waliowaokoa mikononi mwa watu hao waliowateka nyara.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ndipo Mwenyezi-Mungu akawapa waamuzi ambao waliwaokoa mikononi mwa watu waliopora mali zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ndipo Mwenyezi-Mungu akawapa waamuzi ambao waliwaokoa mikononi mwa watu waliopora mali zao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ndipo Mwenyezi-Mungu akawapa waamuzi ambao waliwaokoa mikononi mwa watu waliopora mali zao.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ndipo Mwenyezi Mungu akawainua waamuzi, ambao waliwaokoa kutoka mikononi mwa hao wavamizi.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ndipo bwana akawainua waamuzi, ambao waliwaokoa katika mikono ya hao watu waliowashambulia.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kisha BWANA akawainua waamuzi, waliowaokoa mikononi mwa watu hao waliowateka nyara.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Waamuzi 2:16
14 Marejeleo ya Msalaba  

naam, kama ilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena BWANA anakuambia ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.


Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.


baada ya hayo akawapa waamuzi hata wakati wa nabii Samweli.


Baada yake Abimeleki, akainuka Tola mwana wa Pua, mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, kuwaokoa Israeli; naye alikuwa akikaa Shamiri, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu.


Basi Yeftha akavuka kuwaendea wana wa Amoni ili kupigana nao; naye BWANA akawaua mkononi mwake.


Lakini wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi.


Tena baada ya Ehudi alikuwapo Shamgari mwana wa Anathi, aliyewaua Wafilisti watu mia sita kwa fimbo ya kuswagia ng'ombe; naye aliwaokoa Israeli.


Naye alikuwa akikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.


BWANA akamtazama, akasema, Nenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?


Hapo zamani Waamuzi walipokuwa wanatawala, njaa ilitokea katika nchi. Mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaondoka akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili.


BWANA akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi kutoka kwa mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama.


Naye kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa mikono ya waliowateka nyara.