Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; nao wakamwambia Daudi, hutaingia humu kamwe; maana hata vipofu na viwete watakufukuzia mbali; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
Waamuzi 19:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda kadhaa waliotandikwa; suria wake naye alikuwa pamoja naye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini huyo mtu alikataa kulala huko usiku huo. Basi, akainuka, akaondoka akafika karibu na mji wa Yebusi (yaani Yerusalemu). Alikuwa na wale punda wake wawili waliotandikwa tayari, pamoja na suria wake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini huyo mtu alikataa kulala huko usiku huo. Basi, akainuka, akaondoka akafika karibu na mji wa Yebusi (yaani Yerusalemu). Alikuwa na wale punda wake wawili waliotandikwa tayari, pamoja na suria wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini huyo mtu alikataa kulala huko usiku huo. Basi, akainuka, akaondoka akafika karibu na mji wa Yebusi (yaani Yerusalemu). Alikuwa na wale punda wake wawili waliotandikwa tayari, pamoja na suria wake. Neno: Bibilia Takatifu Lakini akakataa kulala tena, akaondoka na kuelekea Yebusi (ndio Yerusalemu), akiwa na punda wake wawili waliotandikwa, pamoja na suria wake. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini akakataa kulala tena, akaondoka na kwenda mpaka Yebusi (ndio Yerusalemu), akiwa na punda wake wawili waliotandikiwa, pamoja na suria wake. BIBLIA KISWAHILI Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda kadhaa waliotandikwa; suria wake naye alikuwa pamoja naye. |
Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; nao wakamwambia Daudi, hutaingia humu kamwe; maana hata vipofu na viwete watakufukuzia mbali; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.
kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;
na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kufuata jamaa zao.
Kisha wana wa Yuda wakapigana na Yerusalemu, wakautwaa, wakaupiga kwa makali ya upanga, na kuupiga moto huo mji.
Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria wake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu.