Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Waamuzi 18:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Akasema, Ninyi mmeichukua miungu niliyoifanya, na huyo kuhani, nanyi mmekwenda zenu, nami nina nini tena? Basi imekuwaje ninyi kuniuliza, Una nini wewe?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mika akasema, “Nyinyi mmechukua miungu yangu niliyojitengenezea, mkamchukua na kuhani wangu, mkaniacha bila chochote. Mnawezaje basi kuniuliza nina shida gani?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mika akasema, “Nyinyi mmechukua miungu yangu niliyojitengenezea, mkamchukua na kuhani wangu, mkaniacha bila chochote. Mnawezaje basi kuniuliza nina shida gani?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mika akasema, “Nyinyi mmechukua miungu yangu niliyojitengenezea, mkamchukua na kuhani wangu, mkaniacha bila chochote. Mnawezaje basi kuniuliza nina shida gani?”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Akawajibu, “Mmechukua miungu niliyoitengeneza, mkamchukua kuhani wangu, nanyi mkaondoka. Nimebaki na nini kingine? Mnawezaje kuniuliza, ‘Una nini wewe?’ ”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Akawajibu, “Mmechukua miungu yote niliyoitengeneza, mkachukua na kuhani wangu, nanyi mkaondoka. Nimebaki na nini kingine? Mnawezaje kuniuliza, ‘Una nini wewe?’ ”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akasema, Ninyi mmeichukua miungu niliyoifanya, na huyo kuhani, nanyi mmekwenda zenu, nami nina nini tena? Basi imekuwaje ninyi kuniuliza, Una nini wewe?

Tazama sura
Tafsiri zingine



Waamuzi 18:24
15 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu?


Basi Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona.


Kwa hiyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Amazia, akamtuma kwake nabii, aliyemwambia, Mbona umeitafuta miungu ya watu, isiyowaokoa watu wao mkononi mwako?


Wazitengenezao watafanana nazo, Sawa na wote wanaozitumainia.


Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu.


Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.


Na Ohola alifanya mambo ya kikahaba alipokuwa wangu; naye alipenda mno wapenzi wake, Waashuri, jirani zake,


Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia Paulo huyo ameshawishi watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba hiyo inayofanywa kwa mikono siyo miungu.


ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wameleweshwa kwa mvinyo ya uasherati wake.


Ndipo Mika akasema, Sasa ninajua ya kwamba BWANA atanitendea mema, kwa kuwa nina Mlawi kama kuhani wangu.


Basi mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya miungu, naye akafanya naivera, na kinyago, akamweka wakfu mmoja miongoni mwa wanawe, akawa kuhani wake.


Wakawapigia kelele wana wa Dani. Nao wakageuza nyuso zao na kumwambia Mika, Una nini wewe, hata ukaja na mkutano namna hii?


Hao wana wa Dani wakamwambia, Hiyo sauti yako isisikike kati yetu, wasije walio na hasira wakakupiga, nawe ukapotewa na uhai wako, pamoja na uhai wa watu wa nyumbani mwako.