Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Na apandaye akaanguka chali.
Waamuzi 18:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Walipokuwa wamekwenda kitambo kizima kutoka nyumba ya Mika, wale watu waliokuwa katika nyumba zilizokuwa karibu na nyumba ya Mika walikutana, wakawaandama na kuwapata hao wana wa Dani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipokuwa wamefika mbali na nyumbani kwa Mika, watu waliokuwa jirani na Mika wakaitwa, wakawafuatia watu wa kabila la Dani wakawafikia. Biblia Habari Njema - BHND Walipokuwa wamefika mbali na nyumbani kwa Mika, watu waliokuwa jirani na Mika wakaitwa, wakawafuatia watu wa kabila la Dani wakawafikia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipokuwa wamefika mbali na nyumbani kwa Mika, watu waliokuwa jirani na Mika wakaitwa, wakawafuatia watu wa kabila la Dani wakawafikia. Neno: Bibilia Takatifu Walipokuwa wamefika mbali toka nyumbani kwa Mika, watu walioishi karibu na Mika walikusanywa pamoja, nao wakawakimbiza Wadani. Neno: Maandiko Matakatifu Walipokuwa wamesafiri umbali kidogo toka nyumbani kwa Mika, watu walioishi karibu na Mika wakaitwa wakakusanyika pamoja, nao wakawafikia Wadani. BIBLIA KISWAHILI Walipokuwa wamekwenda mbali kidogo kutoka nyumba ya Mika, wale watu waliokuwa katika nyumba zilizokuwa karibu na nyumba ya Mika walikutana, wakawaandama na kuwapata hao wana wa Dani. |
Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Na apandaye akaanguka chali.
Basi wakageuka wakaenda zao, lakini watoto wadogo na wanyama wao wa kufugwa, na vyombo vyao, wakawatanguliza mbele yao.
Wakawapigia kelele wana wa Dani. Nao wakageuza nyuso zao na kumwambia Mika, Una nini wewe, hata ukaja na mkutano namna hii?