Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika Gibea, mji wa Finehasi mwanawe, ambao alipewa katika nchi ya vilima ya Efraimu.
Waamuzi 17:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu huyo akatoka katika huo mji, Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa kama mgeni hapo atakapoona mahali; akafikia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hadi nyumba ya huyo Mika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu. Biblia Habari Njema - BHND Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu. Neno: Bibilia Takatifu Huyu kijana akatoka mji huo wa Bethlehemu ya Yuda na kutafuta mahali pengine pa kuishi. Alipokuwa akisafiri, akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya vilima ya Efraimu. Neno: Maandiko Matakatifu Huyu kijana akatoka katika mji huo wa Bethlehemu ya Yuda na kutafuta mahali pengine ambapo angeweza kuishi. Alipokuwa akisafiri, akafika nyumbani kwa Mika katika vilima vya Efraimu. BIBLIA KISWAHILI Mtu huyo akatoka katika huo mji, Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa kama mgeni hapo atakapoona mahali; akafikia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hadi nyumba ya huyo Mika. |
Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika Gibea, mji wa Finehasi mwanawe, ambao alipewa katika nchi ya vilima ya Efraimu.
Huyo Mlawi aliridhika kukaa na mtu huyo; kisha huyo kijana akawa kwake kama wanawe mmojawapo.
Alikuwako mtu kijana mmoja mwanamume aliyetoka Bethlehemu-yuda, wa jamaa ya Yuda, aliyekuwa Mlawi, naye akakaa huko kama mgeni.
Mika akamuuliza, “Umetoka wapi?” Akamwambia, Mimi ni Mlawi wa Bethlehemu-yuda, nami naenda kukaa popote nitakapoona mahali.
Hapo zamani Waamuzi walipokuwa wanatawala, njaa ilitokea katika nchi. Mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaondoka akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili.