Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli.
Waamuzi 17:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hizo hapakuwepo na mfalme katika Israeli. Kila mtu alifanya chochote alichoona ni chema. Biblia Habari Njema - BHND Siku hizo hapakuwepo na mfalme katika Israeli. Kila mtu alifanya chochote alichoona ni chema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hizo hapakuwepo na mfalme katika Israeli. Kila mtu alifanya chochote alichoona ni chema. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku hizo, Waisraeli hawakuwa na mfalme; kila mtu alifanya alivyoona ni vyema machoni pake. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku hizo Israeli hawakuwa na mfalme, kila mmoja akafanya kama alivyoona vyema machoni pake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe. |
Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli.
Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?
Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja.
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; tena katika siku hizo kabila la Wadani wakajitafutia urithi wapate mahali pa kukaa; maana hawakuwa wamepata urithi wao kati ya makabila ya Israeli.
Ikawa katika siku hizo, kulipokuwa hakuna mfalme katika Israeli, alikuwapo Mlawi mmoja aliyekuwa akikaa kama mgeni upande wa mbele wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu, aliyejitwalia suria katika Bethlehemu-yuda.
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya yaliyokuwa ni mema machoni pake mwenyewe.
Wakasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili kuwa katika Israeli, ya kwamba hivi leo kabila moja limepunguka katika Israeli?