Basi si ninyi mlionileta huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.
Waamuzi 17:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mika akamwambia, kaa pamoja nami, uwe kwangu baba, tena kuhani, nami nitakupa fedha kumi kila mwaka, na nguo ya kuvaa, na vyakula. Basi huyo Mlawi akaingia ndani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mika akamwambia, “Kaa pamoja nami, uwe kwangu kama baba na kuhani wangu. Nitakulipa vipande kumi vya fedha kila mwaka na mavazi pamoja na mahitaji yako.” Biblia Habari Njema - BHND Mika akamwambia, “Kaa pamoja nami, uwe kwangu kama baba na kuhani wangu. Nitakulipa vipande kumi vya fedha kila mwaka na mavazi pamoja na mahitaji yako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mika akamwambia, “Kaa pamoja nami, uwe kwangu kama baba na kuhani wangu. Nitakulipa vipande kumi vya fedha kila mwaka na mavazi pamoja na mahitaji yako.” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Mika akamwambia, “Ishi pamoja nami, uwe baba yangu na kuhani wangu, nami nitakupa shekeli kumi za fedha kila mwaka, pamoja na nguo na chakula.” Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Mika akamwambia, “Ishi pamoja nami, uwe baba yangu na kuhani wangu, nami nitakupa shekeli kumi za fedha, nguo na chakula.” BIBLIA KISWAHILI Mika akamwambia, kaa pamoja nami, uwe kwangu baba, tena kuhani, nami nitakupa fedha kumi kila mwaka, na nguo ya kuvaa, na vyakula. Basi huyo Mlawi akaingia ndani. |
Basi si ninyi mlionileta huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.
Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili.
Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige?
nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako; naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa nyumba ya Yuda.
Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo.
akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwizi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
Huyo Mlawi aliridhika kukaa na mtu huyo; kisha huyo kijana akawa kwake kama wanawe mmojawapo.
Mika akamuuliza, “Umetoka wapi?” Akamwambia, Mimi ni Mlawi wa Bethlehemu-yuda, nami naenda kukaa popote nitakapoona mahali.
Naye akawaambia, Hivi na hivi ndivyo alivyonifanyia Mika, ameniajiri, nami nimekuwa kuhani wake.
Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali nitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate.