Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao;
Waamuzi 16:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nywele zake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nywele zake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nywele zake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. Neno: Bibilia Takatifu Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati huo nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa. BIBLIA KISWAHILI Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake. |
Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao;
Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,
Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.