Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
Waamuzi 16:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku moja Samsoni alikwenda mjini Gaza, akakutana na malaya mmoja akalala naye. Biblia Habari Njema - BHND Siku moja Samsoni alikwenda mjini Gaza, akakutana na malaya mmoja akalala naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku moja Samsoni alikwenda mjini Gaza, akakutana na malaya mmoja akalala naye. Neno: Bibilia Takatifu Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. Neno: Maandiko Matakatifu Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. BIBLIA KISWAHILI Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. |
Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kuu na pwani yake.
Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake.
Samsoni akateremka hadi Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti.
Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.