Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Waamuzi 14:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la BWANA; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Wazazi wake hawakujua kwamba huo ulikuwa mpango wa Mwenyezi-Mungu ambaye alikuwa anatafuta kisa cha kuchukua hatua dhidi ya Wafilisti. Wakati huo, Wafilisti waliwatawala Waisraeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Wazazi wake hawakujua kwamba huo ulikuwa mpango wa Mwenyezi-Mungu ambaye alikuwa anatafuta kisa cha kuchukua hatua dhidi ya Wafilisti. Wakati huo, Wafilisti waliwatawala Waisraeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Wazazi wake hawakujua kwamba huo ulikuwa mpango wa Mwenyezi-Mungu ambaye alikuwa anatafuta kisa cha kuchukua hatua dhidi ya Wafilisti. Wakati huo, Wafilisti waliwatawala Waisraeli.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

(Baba yake na mama yake hawakujua kuwa jambo hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu, kwani alikuwa akitafuta sababu ya kukabiliana na Wafilisti; kwa kuwa wakati huo walikuwa wakiwatawala Waisraeli.)

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

(Baba yake na mama yake hawakujua kuwa jambo hili limetoka kwa bwana, kwani alikuwa akitafuta sababu ya kukabiliana na Wafilisti; kwa kuwa wakati huo walikuwa wakiwatawala Waisraeli.)

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la BWANA; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Waamuzi 14:4
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa BWANA, ili alitimize neno lake, BWANA alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.


BWANA asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la BWANA, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la BWANA.


Hata alipokuwa katika kusema nao, tazama, yule aliyetumwa akamshukia; naye akasema, Angalia, mabaya haya yatoka kwa BWANA; kwani mimi kumngojea BWANA tena?


Basi mfalme hakuwasikia watu wale; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.


Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu.


Lakini Amazia hakutaka kusikia, kwa maana hayo yalitoka kwa Mungu, ili awatie mikononi mwao, kwa kuwa wameitafuta miungu ya Edomu.


Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda.


Basi mawaziri na viongozi wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.


kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.


Kwa kuwa lilikuwa ni la BWANA kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile BWANA alivyomwamuru Musa.


Wana wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya BWANA, BWANA akawatia katika mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arubaini.


Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakateremka hadi Timna, walipofika katika mashamba ya mizabibu huko Timna; mara, mwanasimba akamngurumia.


Ndipo watu elfu tatu wa Yuda wakateremka hadi katika ule ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia, Kadiri ile walivyonitenda mimi, ndivyo nilivyowatenda wao.


Samsoni akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia kwa hawa Wafilisti, hapo nitakapowadhuru.