Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
Waamuzi 14:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Msingelima na mtamba wangu, Hamngekitegua kitendawili changu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku hiyo ya saba, kabla ya jua kutua, wakamwambia Samsoni, “Ni kitu gani kitamu kuliko asali? Ni nani mwenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawajibu, “Kama hamngejishughulisha na mtamba wangu hamngeweza kukitegua kitendawili changu.” Biblia Habari Njema - BHND Siku hiyo ya saba, kabla ya jua kutua, wakamwambia Samsoni, “Ni kitu gani kitamu kuliko asali? Ni nani mwenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawajibu, “Kama hamngejishughulisha na mtamba wangu hamngeweza kukitegua kitendawili changu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku hiyo ya saba, kabla ya jua kutua, wakamwambia Samsoni, “Ni kitu gani kitamu kuliko asali? Ni nani mwenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawajibu, “Kama hamngejishughulisha na mtamba wangu hamngeweza kukitegua kitendawili changu.” Neno: Bibilia Takatifu Siku ya saba, kabla ya jua kutua, wanaume wa mji wakamwambia Samsoni, “Ni nini kilicho kitamu kuliko asali? Ni nini chenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawaambia, “Kama hamkulima na mtamba wangu, msingekitegua kitendawili changu.” Neno: Maandiko Matakatifu Siku ya saba kabla ya jua kutua, watu wa mji wakamwambia Samsoni, “Ni nini kitamu kama asali? Ni nini chenye nguvu kama simba?” Samsoni akawaambia, “Kama hamkulima na mtamba wangu, hamngeweza kufumbua kitendawili changu.” BIBLIA KISWAHILI Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho kitamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Msingelima na mtamba wangu, Hamngekitegua kitendawili changu. |
Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.
Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kulia; na hao wanne walikuwa na uso wa ng'ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia.
Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili.
Roho ya BWANA ikamjia juu yake kwa nguvu, naye akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavazi hayo ya sikukuu. Hasira zake zikampanda, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.