Lakini wakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi wala wana wenu, hata milele;
Waamuzi 13:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Asionje mazao yoyote ya mzabibu, wala asinywe divai au kileo wala kula chochote kilicho najisi. Yote niliyomwamuru, ayafuate.” Biblia Habari Njema - BHND Asionje mazao yoyote ya mzabibu, wala asinywe divai au kileo wala kula chochote kilicho najisi. Yote niliyomwamuru, ayafuate.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza asionje mazao yoyote ya mzabibu, wala asinywe divai au kileo wala kula chochote kilicho najisi. Yote niliyomwamuru, ayafuate.” Neno: Bibilia Takatifu Kamwe asile kitu chochote kitakachotoka katika mzabibu, wala asinywe divai yoyote wala kileo chochote, wala asile kitu chochote kilicho najisi. Hana budi kufanya kila kitu nilichomwagiza.” Neno: Maandiko Matakatifu Kamwe asile kitu chochote kitakachotoka katika mzabibu, wala asinywe mvinyo wa aina yoyote wala kileo chochote wala asile kitu chochote kilicho najisi. Hana budi kufanya kila kitu nilichomwagiza.” BIBLIA KISWAHILI Asile kitu chochote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze. |
Lakini wakasema, Hatutakunywa divai; kwa maana Yonadabu, mwana wa Rekabu, baba yetu, alituamuru, akisema, Msinywe divai, ninyi wala wana wenu, hata milele;
Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mwanamume au mwanamke atakapoweka nadhiri maalumu, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa BWANA;
Siku zote za kujitenga kwake asile kitu chochote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda.
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza na kwamba mtaendelea kuyafanya.
Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hadi siku ya kufa kwake.