Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.
Waamuzi 13:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, “Hebu huyo mwanamke ajihadhari na yote niliyomwambia.” Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Mkeo atapaswa kushika yote niliyomwambia: Biblia Habari Njema - BHND Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Mkeo atapaswa kushika yote niliyomwambia: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Mkeo atapaswa kushika yote niliyomwambia: Neno: Bibilia Takatifu Malaika wa Mwenyezi Mungu akamjibu, “Mke wako hana budi kufanya yale yote niliyomwambia. Neno: Maandiko Matakatifu Malaika wa bwana akamjibu, “Mke wako hana budi kufanya yale yote niliyomwambia. BIBLIA KISWAHILI Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, “Hebu huyo mwanamke ajihadhari na yote niliyomwambia.” |
Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.
Basi Manoa akainuka, akamfuata mkewe, na kumfikia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Ndio, ni mimi.
Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini?
Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;