Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Waamuzi 13:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Manoa akasema, “Sasa maneno yako yatakapotimia ni mambo gani tutakayofuata kwa ajili ya huyo mtoto? Tutafanya nini kwa ajili yake?” Biblia Habari Njema - BHND Kisha Manoa akasema, “Sasa maneno yako yatakapotimia ni mambo gani tutakayofuata kwa ajili ya huyo mtoto? Tutafanya nini kwa ajili yake?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Manoa akasema, “Sasa maneno yako yatakapotimia ni mambo gani tutakayofuata kwa ajili ya huyo mtoto? Tutafanya nini kwa ajili yake?” Neno: Bibilia Takatifu Basi Manoa akamuuliza, “Maneno yako yatakapotimia, je, masharti ya maisha ya mtoto huyu yatakuwa ni yapi, na kazi yake itakuwa ni ipi?” Neno: Maandiko Matakatifu Basi Manoa akamuuliza, “Wakati maneno yako yatakapotimia, masharti ya maisha ya mtoto huyu yatakuwa nini na kazi yake itakuwa ni nini?” BIBLIA KISWAHILI Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini? |
Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.
Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.
Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Basi Manoa akainuka, akamfuata mkewe, na kumfikia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Ndio, ni mimi.
Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, “Hebu huyo mwanamke ajihadhari na yote niliyomwambia.”