Waamuzi 12:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Baada ya Yeftha, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya Yeftha, Ibzani kutoka Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya Yeftha, Ibzani kutoka Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya Yeftha, Ibzani kutoka Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. BIBLIA KISWAHILI Baada ya Yeftha, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi wa Israeli. |
Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, majusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
Baada yake Abimeleki, akainuka Tola mwana wa Pua, mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, kuwaokoa Israeli; naye alikuwa akikaa Shamiri, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu.
Huyo Yeftha akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka sita. Ndipo akafa Yeftha, Mgileadi, akazikwa katika miji ya Gileadi mmojawapo.
Alikuwa na watoto thelathini wa kiume; na binti thelathini aliwaoza nje ya ukoo wake, kisha akaleta wanawake thelathini kutoka mahali pengine kwa ajili ya hao wanawe. Akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka saba.
Alikuwako mtu kijana mmoja mwanamume aliyetoka Bethlehemu-yuda, wa jamaa ya Yuda, aliyekuwa Mlawi, naye akakaa huko kama mgeni.
Ikawa katika siku hizo, kulipokuwa hakuna mfalme katika Israeli, alikuwapo Mlawi mmoja aliyekuwa akikaa kama mgeni upande wa mbele wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu, aliyejitwalia suria katika Bethlehemu-yuda.
BWANA akamwambia Samweli, utamlilia Sauli hadi lini, kwa kuwa mimi nimemkataa asiwatawale Waisraeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakutuma kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.