Waamuzi 11:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawapiga kutoka Aroeri hadi kufikia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa pigo kuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akajipatia ushindi mkubwa, akateka maeneo ishirini yaliyokuwa kati ya Aroeri, sehemu zilizozunguka Minithi na Abel-keramimu. Basi Waamoni wakashindwa kabisa na Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Akajipatia ushindi mkubwa, akateka maeneo ishirini yaliyokuwa kati ya Aroeri, sehemu zilizozunguka Minithi na Abel-keramimu. Basi Waamoni wakashindwa kabisa na Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akajipatia ushindi mkubwa, akateka maeneo ishirini yaliyokuwa kati ya Aroeri, sehemu zilizozunguka Minithi na Abel-keramimu. Basi Waamoni wakashindwa kabisa na Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu Akaharibu kabisa miji ishirini kuanzia Aroeri hadi karibu na Minithi, na kuendelea hadi Abel-Keramimu. Hivyo, Waisraeli wakawashinda Waamoni. Neno: Maandiko Matakatifu Akawapiga kwa ushindi mkubwa kuanzia Aroeri mpaka karibu na Minithi na kuendelea mpaka Abel-Keramimu, miji yote iliyopigwa ni ishirini. Basi Israeli wakawashinda Waamoni. BIBLIA KISWAHILI Akawapiga kutoka Aroeri hadi kufikia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa pigo kuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli. |
Yuda, na nchi ya Israeli, walikuwa wachuuzi wako; walitoa badala ya bidhaa yako ngano ya Minithi, na mtama, na asali, na mafuta, na zeri.
Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa na ngome ndefu ya kutushinda; BWANA, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisongelea;
Basi Yeftha akavuka kuwaendea wana wa Amoni ili kupigana nao; naye BWANA akawaua mkononi mwake.