Lakini Amazia hakutaka kusikia. Basi Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea; wakatazamana uso kwa uso, yeye na Amazia mfalme wa Yuda, huko Beth-shemeshi ulio wa Yuda.
Waamuzi 11:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini mfalme wa wana wa Amoni hakuusikiza ujumbe aliotumiwa na Yeftha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mfalme wa Amoni alipuuza ujumbe huo wa Yeftha. Biblia Habari Njema - BHND Lakini mfalme wa Amoni alipuuza ujumbe huo wa Yeftha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mfalme wa Amoni alipuuza ujumbe huo wa Yeftha. Neno: Bibilia Takatifu Hata hivyo, mfalme wa Waamoni hakuyajali maneno ya ujumbe wa Yefta. Neno: Maandiko Matakatifu Hata hivyo, Mfalme wa Waamoni, hakuyajali maneno ya ujumbe wa Yefta. BIBLIA KISWAHILI Lakini mfalme wa wana wa Amoni hakuusikiliza ujumbe aliotumiwa na Yeftha. |
Lakini Amazia hakutaka kusikia. Basi Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea; wakatazamana uso kwa uso, yeye na Amazia mfalme wa Yuda, huko Beth-shemeshi ulio wa Yuda.
Basi mimi sikukufanyia wewe dhambi, lakini wewe unanitenda uovu kwa kupigana nami; yeye BWANA, yeye Mwamuzi, na awe mwamuzi hivi leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni.
Ndipo Roho ya BWANA ikamjia Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni.