Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Waamuzi 11:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi mimi sikukufanyia wewe dhambi, lakini wewe unanitenda uovu kwa kupigana nami; yeye BWANA, yeye Mwamuzi, na awe mwamuzi hivi leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mimi sijakukosea kitu na ndio maana unafanya kosa unaponishambulia. Mwenyezi-Mungu ambaye ndiye Mwamuzi ataamua leo hii kati ya Waisraeli na watu wa Amoni.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mimi sijakukosea kitu na ndio maana unafanya kosa unaponishambulia. Mwenyezi-Mungu ambaye ndiye Mwamuzi ataamua leo hii kati ya Waisraeli na watu wa Amoni.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mimi sijakukosea kitu na ndio maana unafanya kosa unaponishambulia. Mwenyezi-Mungu ambaye ndiye Mwamuzi ataamua leo hii kati ya Waisraeli na watu wa Amoni.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mimi sijakukosea, bali wewe ndiwe unanikosea kwa kufanya vita nami. Basi Mwenyezi Mungu, aliye Mwamuzi, leo na aamue ugomvi kati ya Waisraeli na Waamoni.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mimi sijakukosea jambo lolote, bali wewe ndiye unayenikosea kwa kufanya vita nami. Basi bwana, aliye Mwamuzi, leo na aamue ugomvi kati ya Waisraeli na Waamoni.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi mimi sikukufanyia wewe dhambi, lakini wewe unanitenda uovu kwa kupigana nami; yeye BWANA, yeye Mwamuzi, na awe mwamuzi hivi leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Waamuzi 11:27
27 Marejeleo ya Msalaba  

Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.


La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?


Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu. Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake.


Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yanatazama kwako.


Hapo waelekevu wangepata kuhojiana naye; Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.


Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, siwezi kumjibu; Ni lazima nimwombe mshitaki wangu anihurumie.


Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.


Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu akasirikiaye waovu kila siku.


Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.


Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana mataifa yote ni yako.


Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze, Uwape wenye kiburi stahili zao.


Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.


Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.


Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.


Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee malipo ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, yawe ni mema au mabaya.


baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.


mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,


Lakini mfalme wa wana wa Amoni hakuusikiza ujumbe aliotumiwa na Yeftha.


Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.


BWANA atuamue, mimi na wewe, na BWANA anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.


Kama vile walivyosema watu wa kale katika mithali yao, Katika waovu hutoka uovu; ila mkono wangu hautakuwa juu yako.


Basi BWANA atuamue, akatuhukumu mimi na wewe, akaone, akanitetee neno langu, akaniokoe kutokana na mkono wako.


Ikawa, Daudi alipokwisha kumwambia Sauli maneno hayo Sauli alisema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Naye Sauli akapaza sauti yake, akalia.