Waamuzi 1:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa. Biblia Habari Njema - BHND Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa. Neno: Bibilia Takatifu Waamori pia walikuwa wameamua kuendelea kuishi katika Mlima Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu; lakini nguvu ya nyumba ya Yusufu ilipoongezeka, wao pia wakashindwa na wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa. Neno: Maandiko Matakatifu Waamori pia wakaendelea kukaa katika Mlima Heresi, katika Aiyaloni na Shaalbimu, lakini mkono wa nyumba ya Yusufu ukawalemea, nao wakashindwa hata wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa. BIBLIA KISWAHILI lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa. |
watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.
Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
Kisha Waamori waliwasukumiza wana wa Dani waende milimani; kwani hawakuwakubali kuteremkia bondeni;