Ndipo BWANA akanilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
Waamuzi 1:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Beth-shemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya, hao wenyeji wa Beth-shemeshi, na wenyeji wa Bethi-anathi, wakawatumikia kazi ya shokoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa kabila la Naftali hawakuwafukuza wakazi wa mji wa Beth-shemeshi au wakazi wa Beth-anathi, lakini walikaa pamoja nao. Hata hivyo wenyeji wa miji hiyo, walilazimishwa kuwafanyia Waisraeli kazi za kulazimishwa. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa kabila la Naftali hawakuwafukuza wakazi wa mji wa Beth-shemeshi au wakazi wa Beth-anathi, lakini walikaa pamoja nao. Hata hivyo wenyeji wa miji hiyo, walilazimishwa kuwafanyia Waisraeli kazi za kulazimishwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa kabila la Naftali hawakuwafukuza wakazi wa mji wa Beth-shemeshi au wakazi wa Beth-anathi, lakini walikaa pamoja nao. Hata hivyo wenyeji wa miji hiyo, walilazimishwa kuwafanyia Waisraeli kazi za kulazimishwa. Neno: Bibilia Takatifu Wala Naftali hawakuwafukuza wale walioishi Beth-Shemeshi wala wale walioishi Beth-Anathi; lakini Naftali nao pia wakaishi miongoni mwa Wakanaani, wenyeji wa nchi, nao wale walioishi Beth-Shemeshi na Beth-Anathi wakawa watumishi wao katika kazi ya kulazimishwa. Neno: Maandiko Matakatifu Wala Naftali hawakuwafukuza wale walioishi Beth-Shemeshi wala wale walioishi Beth-Anathi; lakini Naftali nao pia wakaishi miongoni mwa Wakanaani, wenyeji wa nchi, nao wale walioishi Beth-Shemeshi na Beth-Anathi wakawa watumishi wao katika kazi ya kulazimishwa. BIBLIA KISWAHILI Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Beth-shemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya, hao wenyeji wa Beth-shemeshi, na wenyeji wa Bethi-anathi, wakawatumikia kazi ya shokoa. |
Ndipo BWANA akanilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hadi kilima Seiri, kisha ukaendelea hadi upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukateremkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;
Zabuloni naye hakuwatoa wenyeji wa Kitroni, wala hao waliokaa katika Nahalali; lakini Wakanaani walikaa kati yao, wakalazimishwa shokoa.
lakini Waasheri wakakaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; kwa kuwa hawakuwafukuza.
Kisha Waamori waliwasukumiza wana wa Dani waende milimani; kwani hawakuwakubali kuteremkia bondeni;
lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa.