Waamuzi 1:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha Yuda akaenda pamoja na nduguye Simeoni, na wakawapiga Wakanaani waliokaa katika Sefathi, na kuuharibu mji kabisa. Na jina la mji huo ulikuwa ukiitwa Horma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa kabila la Yuda walishirikiana na ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, wakawashinda Wakanaani waliokaa Sefathi. Waliuangamiza kabisa mji huo na kugeuza jina lake kuwa Horma. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa kabila la Yuda walishirikiana na ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, wakawashinda Wakanaani waliokaa Sefathi. Waliuangamiza kabisa mji huo na kugeuza jina lake kuwa Horma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa kabila la Yuda walishirikiana na ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, wakawashinda Wakanaani waliokaa Sefathi. Waliuangamiza kabisa mji huo na kugeuza jina lake kuwa Horma. Neno: Bibilia Takatifu Basi wanaume wa Yuda wakaenda na Wasimeoni ndugu zao, wakawashambulia Wakanaani walioishi Sefathi, nao wakauangamiza huo mji kabisa. Kwa hiyo huo mji ukaitwa Horma. Neno: Maandiko Matakatifu Basi watu wa Yuda wakaenda na Wasimeoni ndugu zao kushambulia Wakanaani waishio Sefathi, nao wakauangamiza huo mji kabisa. Kwa hiyo huo mji ukaitwa Horma BIBLIA KISWAHILI Kisha Yuda akaenda pamoja na nduguye Simeoni, na wakawapiga Wakanaani waliokaa katika Sefathi, na kuuharibu mji kabisa. Na jina la mji huo ulikuwa ukiitwa Horma. |
Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakateremka, wakawapiga na kuwaangusha, hadi wakafika Horma.
BWANA akasikiza sauti ya Israeli, akawatia Wakanaani mikononi mwao; nao wakawaharibu wao na miji yao kabisa; na jina la mahali hapo likaitwa Horma.
Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika eneo langu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika eneo lako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye.