Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,
Ufunuo 8:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Mwana-kondoo alipofungua mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa kama nusu saa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. Biblia Habari Njema - BHND Na Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. Neno: Bibilia Takatifu Mwana-Kondoo alipouvunja ule muhuri wa saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. Neno: Maandiko Matakatifu Mwana-Kondoo alipoivunja ile lakiri ya saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. BIBLIA KISWAHILI Na Mwana-kondoo alipofungua mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa kama nusu saa. |
Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,
Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.
Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.
Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe mhuri, pamoja na kuwaweka wale askari walinzi.
Kisha nikaona katika mkono wa kulia wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba.
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Kisha nikaona Mwana-kondoo alipofungua mojawapo ya ile mihuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo!
Nami nikaona, alipoufungua mhuri wa sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
Na alipoufungua mhuri wa tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
Na alipoufungua mhuri wa tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.