Lakini nenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utaamka katika kura yako mwisho wa siku hizo.
Ufunuo 6:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wasubiri bado muda mchache, hadi itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu zao, watakaouawa kama wao walivyouawa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakapewa kila mmoja vazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu ambao watauawa kama wao wenyewe walivyouawa. Biblia Habari Njema - BHND Wakapewa kila mmoja vazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu ambao watauawa kama wao wenyewe walivyouawa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakapewa kila mmoja vazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu ambao watauawa kama wao wenyewe walivyouawa. Neno: Bibilia Takatifu Kisha kila mmoja wao akapewa joho jeupe na wakaambiwa wangoje kwa muda kidogo zaidi, hadi idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouawa kama wao walivyouawa, itakapotimia. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha kila mmoja wao akapewa joho jeupe na wakaambiwa wangoje kwa muda kidogo zaidi, mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouawa kama wao walivyouawa, itakapotimia. BIBLIA KISWAHILI Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wasubiri bado muda mchache, hadi itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu zao, watakaouawa kama wao walivyouawa. |
Lakini nenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utaamka katika kura yako mwisho wa siku hizo.
Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwaua.
Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
Watawatenga na masinagogi; naam, saa inakuja kila mtu awauaye atakapodhania ya kuwa anamfanyia Mungu ibada.
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,
kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.
mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,
Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake.
akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na kukawia tena baada ya haya;
Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, ili ile sanamu ya mnyama iongee, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu sana.
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.
Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;