Ufunuo 19:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye amevikwa vazi lililoloweshwa katika damu, na jina lake anaitwa, Neno la Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alikuwa amevaa vazi lililokuwa limelowekwa katika damu. Na jina lake huyo ni “Neno la Mungu”. Biblia Habari Njema - BHND Alikuwa amevaa vazi lililokuwa limelowekwa katika damu. Na jina lake huyo ni “Neno la Mungu”. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alikuwa amevaa vazi lililokuwa limelowekwa katika damu. Na jina lake huyo ni “Neno la Mungu”. Neno: Bibilia Takatifu Amevaa joho lililoloweshwa katika damu, na Jina lake ni Neno la Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Amevaa joho lililochoviwa katika damu, na Jina lake ni “Neno la Mungu.” BIBLIA KISWAHILI Naye amevikwa vazi lililoloweshwa katika damu, na jina lake anaitwa, Neno la Mungu. |
Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyovingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kuhusu Neno la uzima;
Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili.