Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya;
Ufunuo 17:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shabaha ya hawa kumi ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote. Biblia Habari Njema - BHND Shabaha ya hawa kumi ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shabaha ya hawa kumi ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote. Neno: Bibilia Takatifu Hawa wana nia moja, nao watamwachia yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. Neno: Maandiko Matakatifu Hawa wana nia moja, nao watamwachia yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. BIBLIA KISWAHILI Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. |
Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya;
Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;
ijalizeni furaha yangu, ili muwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkiwaza mamoja.
Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.