Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Ufunuo 10:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Na ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nilikuwa tayari kuandika. Nami nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie mhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Na hizo ngurumo saba ziliposema, mimi nikataka kuandika. Lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni: “Maneno ya ngurumo hizo saba ni siri; usiyaandike!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Na hizo ngurumo saba ziliposema, mimi nikataka kuandika. Lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni: “Maneno ya ngurumo hizo saba ni siri; usiyaandike!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Na hizo ngurumo saba ziliposema, mimi nikataka kuandika. Lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni: “Maneno ya ngurumo hizo saba ni siri; usiyaandike!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nazo zile radi saba zilipotoa ngurumo, nilitaka kuanza kuandika, lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Yatie muhuri hayo yaliyosemwa na hizo radi saba na usiyaandike.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Nazo zile radi saba zilipotoa ngurumo, nilitaka kuanza kuandika, lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Yatie muhuri hayo yaliyosemwa na hizo radi saba na usiyaandike.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nilikuwa tayari kuandika. Nami nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie mhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Ufunuo 10:4
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya kitabu kilichotiwa mhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa mhuri;

BWANA akaniambia, Ujipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa hati ya kawaida, Kwa Maher-shalal-hash-bazi;

Ufunge huo ushuhuda, ukaitie mhuri sheria kati ya wanafunzi wangu.

Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.

Akasema, Nenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa mhuri, hata wakati wa mwisho.

Na maono ya hizo nyakati za jioni na asubuhi yaliyosemwa ni kweli; lakini wewe yafunike maono hayo; maana ni ya wakati ujao baada ya siku nyingi.

Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.

ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika kitabu, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Nenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.

Akaniambia, Usiyatie mhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.